Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeitupilia mbali kesi ya madai iliyokuwa inamkabili  Askofu wa kanisa la Efatha, Josephat Mwingira iliyofunguliwa na Dk William Morris, raia wa Marekani dhidi ya mkewe Dk Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira kwa kuwa na mahusiano na kuzaa mtoto aliyejulikana kwa jina la Daudi.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambaye amesema Dk Morris ameshindwa kuthibitisha uhusiano wa kimapenzi  kati ya Dk Phills na Mchungaji Mwingira pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa ni matokeo ya uhusiano wa kimapenzi kati ya Dh Phills na Mchungaji Mwingira.

Awali katika utetezi wa Dk Phills Nyimbi, aliieleza mahakama hiyo kuwa hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Josephat Mwingira, na mtoto aliyezaliwa alikili kuwa amezaa nje ya ndoa lakini si na Mchungaji Mwingira.

Akiongozwa na Wakili Peter Swai kutoa ushahidi katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyekuwa mumewe ambaye ni raia wa Marekani, Dk William Morris, Dk Nyimbi aliomba mwanaume huyo asilipwe kiasi cha fedha cha Sh7.5 bilioni anazodai kwa sababu hakuwa na uhusiano na Mchungaji Mwingira.

Disemba 28, 2011,  Dk Morris na Dk Phills walifunga ndoa ya Kanisani na wakati wa uhusiano wao, Dk Phillis na Mchungaji Mwingira wanadaiwa  kuingia katika uhusiano wa mapenzi na kubahatika kupata  mtoto wa kiume ambaye kwa sasa ana umri wa miaka tisa.

Kamanda Mambosasa: Kitakacho wakuta tusilaumiane
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 27, 2018