Wananchi wa Urusi wamepiga kwa kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba, juu yamchakato wa kumruhusu Rais Vladimir Putin kuwania mihula miwili zaidi madarakani, ambayo itambakisha madarakani hadi mwaka 2036.

Upigaji wa kura ya mapema umefanyika katika maeneo yote ya Nchi hiyo jana, siku moja baada ya gwaride kubwa la kijeshi kuadhimisha miaka 75 baada ya kumalizika vita vya pili vya Dunia.

Ingawa umaarufu wake umeporomoka kutokana na athari za janga la virusi vya corona, Putin mwenye umri wa miaka 67 bado anao uungwaji mkono mkubwa nchini Urusi.

Zoezi hili la kura ya maoni ambalo linatarajiwa kukamilika Jumatano ijayo, linatarajiwa kuidhinisha mabadiliko ya katiba yaliyopendekezwa na serikali ya Rais Putin.

Uchaguzi Malawi: Upinzani waongoza matokeo ya awali
Kocha Sven: Tuna kazi ya kusaka pointi tatu kutimiza malengo