Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya aliyejizolea kundi kubwa la mashabiki kutoka pembe zote za ukanda wa Afrika mashariki Vinnie Bite, ametangaza rasmi kuwa mtangazaji mpya wa kituo cha redio Milele fm Kenya.

Nyota huyo wa ucheshi ameshiriki habari hiyo njema na mashabiki wake kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, akiwaarifu kuwa wakae tayari kumpata kupitia upande huo mwingine wa kazi yake mpya ambapo atakuwa akisikika katika mfululizo wa vipindi vya wiki nzima.

Vinnie anaingia kujiunga kwenye kipindi kimoja na mtangazaji mkongwe nchini Kenya Francis Luchivya.

“God above everything, Sasa mimi ni Radio presenter but hauwezi elewa Tune in to Milele Fm from mon-fri every week tupepete iwake tukiwa na bigman Luchivya,” ameshiriki Vinnie.

Taarifa za mchekeshaji huyo kujiunga na kituo cha radio inakuja muda mfupi baada ya mchekeshaji mwezie David Oyado maarufu Mulamwah kutangazwa kujiunga na kituo hicho pia.

Jumatatu Mei 16, 2022, alidokeza shauku na matamanio yake ya muda mrefu kuhusu kupata nafasi ya kuwa mfanyakazi wa radio na hatimaye ndoto zake zimetimia.

“Mungu ni mkubwa, hatimaye niko kwenye Radio, Muda wote ilikuwa ni ndoto yangu siku moja nifanye kazi redioni, Ahsante kwa mashabiki wangu ambao muda wote mliniamini na kuniunga mkono.” aliongeza.

Habari Kuu katika magazeti ya leo Mei 19, 2022. 
Muna Love adhihirisha uchungu wa kuzushiwa kifo