Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Alfred Nombo (28) kwa kosa la kuumuua Erasto Nchimbi (28) mkazi wa Kijiji cha Sara, Wilayani Mbinga kwa kumchoma na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma Simon Maigwa amewaambia waandishi wa habari leo kuwa tukio hilo limetokea Mei 19 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi.

Alisema kuwa Nombo alikuwa na wivu wa kimapenzi kwa mke wa Nchimbi na kuamua kumuua kwa kumchoma na kisu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda Maigwa alisema kuwa Nombo alinogewa na mapenzi ya mke wa marehemu Nchimbi kiasi cha kupelekea kuvunja ndoa yao  na wivu uliomfanya afanye maamuzi ya kumuuwa mwenye mke ili apate nafasi ya kuwa huru na mke wa Nchimbi.

Aidha Kamanda Maigwa ametoa wito kwa watu wenye uhasama kupeleka matatizo yao katika vyombo vya usuluhishi badala ya kujichukulia maamuzi ambayo yanagharimu maisha ya watu na kuishia jela.

Hunt afafanua kipigo cha Azam FC kabla ya kuivaa Simba SC
Jonas Mkude shakani Simba SC