Mchezaji na mwongozaji sinema maarufu wa India, Shashi Kapoor amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79 nchini humo.

Shashi ambaye alikuwa mmoja wa familia maarufu ya Kapoor ambayo imekuwa katika tasnia ya filamu nchini India kwa miaka mingi.

Aidha, msanii huyo ambaye alicheza katika sinema nyingi za India zikiwemo filamu maarufu kama vile, Deewar na Kabhie Kabhie alikuwa hospitalini kwa muda mrefu akiuguzwa.

Vile vile, amewahi kushinda tuzo mbalimbali za filamu na serikali ya India iliwahi kumpa tuzo maalum ya kiraia inayojulikana kama Padma Bhushan mwaka 2011.

Hata hivyo, msanii huyo aliwahi kucheza sinema kadhaa na muigizaji mwingine mkubwa wa India Amitabh Bachchan katika baadhi ya filamu kubwa kubwa kutoka India katika miaka ya 1970, wakicheza mara nyingine kama ndugu, marafiki na kama maadui.

Chadema: Wema hafai hata kupewa ujumbe wa nyumba kumi
Rais auawa kwa kupigwa risasi