Jarida la French (France Football) limetangaza kufanya mabadiliko ya mtiririko wa kumpata mchezaji bora wa mwaka, baada ya mkataba wao na shirikisho la soka duniani FIFA uliodumu kwa miaka sita kufikia kikomo.

France Football wamebadilisha washiriki katika upigaji wa kura kwa kuwaondoa mameneja wa klabu pamoja na wachezaji.

Mfumo wa kuwahusisha washiriki hao ulianza kutumia mwaka 2009 baada ya kuwepo kwa makubaliano kati ya jarida hilo ambalo lina haki miliki na jina na Ballon d’Or pamoja na FIFA ambao hapo awali walikua wakisimamia shughuli za kumpata mchezaji bora wa dunia kwa jina la (FIFA World Player of the Year award).

Uwepo wa washirikia hao ulionekana kuchangia ushindani uliopo tangu mwaka 2009, kati ya Lionel Messi aliyeshinda tuzo hiyo mara nne dhidi ya Cristiano Ronaldo aliyeshinda mara tatu.

Kabla ya mwaka 1995 Ballon d’Or ilikua inajihusuisha na wachezaji wa soka wa barani Ulaya, lakini baadae walibadilisha na kuwahusha wachezaji wengine kutoka kwenye mabara mengine duniani.

Maamuzi yaliyofanywa upande wa wapiga kura ni kuibakishwa kwa waandishi wa habari pekee ambao watahusika na zoezi hilo, huku orodha ya wachezaji watakaoingia kwenye kinyang’anyiro ikiongezwa kutoka 23 hadi 30 na mwishowe itapunguzwa na kufikia wachezaji watatu ambao watawania tuzo hiyo.

Pia wamejipanga kumpata mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or kabla ya kumalizika kwa mwaka husika, tofauti na ilivyo sasa mchezaji wa mwaka husika hutangazwa mwanzoni mwa mwaka unaofuata (Januari).

Hata hivyo mabadiliko hayo bado hayajaungwa mkono na shirikisho la soka duniani FIFA, jambo ambalo limeanza kuhisiwa huenda wakaandaa utaratibu wao mwingine na kusababisha uwepo wa tuzo mbili tofauti.

FIFA walikua wakiendesha zoezi la utoaji wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka (FIFA World Player of the Year) tangu mwaka 1991 hadi 2008 ambapo walikubali kuungana na Jarida la French (France Football) waliokua na shughuli za kuratibu tuzo ya Ballon d’Or.

Gundogan: Klopp Alinishauri Kujiunga Man City
Pako Ayesteran Afungasha Virago, Voro Bosi Wa Muda