Mchezaji kutoka nchini Brazil, Wergiton do Rosalio Calmon amejiunga na Klabu ya Al- Shabab ya nchini Saudi Arabia ili kuweza kuitumikia klabu hiyo.

Wergiton do Rosario Calmon amechezea katika klabu ya Ufaransa ya Toulouse kwa takriban miaka mitatu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka Brazil sasa amehamia katika klabu ya Al-Shabab yenye maskani yake nchini Saudia.

Aidha, mitandao ya kijamii imekuwa ikilihusisha jina hilo na kikundi cha waasi cha Al- Shabab kilichopo nchini Somalia.

Kundi hilo linalohusishwa na lile la al-Qaeda limekuwa likipigana na serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa kwa ,muonhgo mmja uliopita na limetekeleza mashambulizi katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.

 

Video: Rais Mstaafu Kikwete akwea Pipa kuelekea nchini Zimbabwe
Video: Makontena ya Makonda yapigwa mnada, Ridhiwani Kikwete aibua taharuki