Huenda Manchester United wakaingia kwenye  hatari ya kumpoteza nyota wao kinda Angel Gomes mwenye mpango wa kwenda ndani ya kikosi cha Barcelona.

Gomez mwenye miaka 19 amesema kuwa ana mpango wa kuondoka ndani ya Old Trafford kwa ajili ya kutimiza malengo yake aliyojiwekea baada ya kushindwa kufikia makubaliano na mabosi wa United.
Kinda huyo anakipiga pia kwenye timu ya taifa ya England ile ya chini ya miaka 20 alianza kulelewa ndani ya United akiwa na miaka sita amecheza jumla ya mechi saba za wakubwa na alianza tatu pekee za kwenye Ligi ya Europa.
Habari zinaeleza kuwa mbali na Barcelona ambako anacheza mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi pia Juventus na Craystal Palace zimeonyesha nia ya kuipata saini ya kinda huyo.

Aiba fedha benki na kuwarushia wapita njia akiwatakia ‘Heri ya Krismas’
Jeshi la Polisi Kenya limewataka Wananchi kuwa makini msimu wa sikukuu