Mchezo namba 202 wa Ligi kuu Tanzania Bara kati ya Lipuli FC ya Iringa dhidi ya vinara wa ligi, Simba SC uliopangwa kuchezwa April 20, 2018 kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa umepelekwa mbele na hatimaye kuchezwa April 21 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura na kusema sababu kubwa ya kusogezwa mbele mchezo huo ni kutokana na wamiliki wa uwanja huo kuwa na shughuli ya kijamii kwenye uwanja siku ya April 20.

Aidha, Simba inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumamosi huku ikiwa na alama 58 pekee ambapo inaifanya timu hiyo mpaka sasa kuendelea kushika usukani wa ligi, nafasi ya pili ikichukuliwa na watani wao jadi Yanga kwa alama 47, Azam FC akishika nafasi ya tatu kwa alama 46

Mwanamke amshtaki Mariah Carey kwa kumnyanyasa kingono
Khaligraph Jones aeleza alivyomkwaruza Octopizzo

Comments

comments