Mchakato wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kupata wagombea katika nafasi mbalimbali unaanza leo ambapo mikutano ya ngazi ya wilaya,majimbo itapiga kura za mapendekezo kati ya leo na kesho.

Upigaji wa kura unaoanza leo unahusisha kura za maoni za kuwapata wagombea katika nafasi za ubunge, uwakilishi, udiwani (Tanzania Bara) na usheha kwenye wadi visiwani Zanzibar.

Wiki iliyopita Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Magufuli alisema zaidi ya wanachama 8000 wamechukua fomu kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM, huku Mkoa wa Dar es salaam ukiongoza kwa kuwa na wagombea wengi zaidi.

Julai 30 kutakuwa na vikao vya kamati za siasa za majimbo kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo kwenye kamati za siasa za wilaya.

Vikao vya uteuzi kwa wagombea ubunge vitafanywa na Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kwa Tanzania Bara na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi ni Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar.

Tamko la Jeshi la polisi Matukio ya moto Shuleni
Bil. 20 zatolewa kulipa madeni ya korosho Mtwara