Bondia Alphonce Mchumiatumbo amesaini mkataba wa kuzipiga na Benki Mwakalebela, januari 30 katika ukumbi wa sativa Kyela Mbeya, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mpambano huwa wa uzani wa juu kufanyika nyanda za juu kusini.

Akisaini mkataba mbele ya Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa amesema atahakikisha kuwa mabondia wa uzito wa juu wanakuwa juu zaidi kwa mapambano hayo katika uzito uho

Chaurembo, ameongeza kwa kusema chama chao kimejizatiti kuinua mchezo wa ngumi kwa kufata taratibu na sheria za mchezo huo wa masumbwi nchini, kwa kuhakikisha kila bondia anapima afya na uzito wake kwa usalama.

Kwa upande wa bondia Alphonce Mchumiatumbo amesema kuwa kwa sasa yupo katika mazoezi mazito chini ya kocha wake Juma Urungu ‘Mkebezi’ ambapo kwa siku amekuwa akifanya mazoezi mara mbili au tatu kwa ajili ya kujiandaa na mpambano huo.

habari hii ni kwa hisani ya  Rajab Muhamila (Super D) 

FIFA Yaitaka Etoile Du Sahel Kuilipa Simba Haraka
Tanzia: Leticia Nyerere afariki