Mchungaji mmoja huko Afrika Kusini amekosolewa vikali baada ya kuanza kubatiza waumini wake kwa kutumia vilevi ambavyo wanavipenda kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu.

Askofu Tsietsi Makiti, (52) ambaye pia  ni Mwanzilishi wa kanisa hilo linalojulikana kama ‘Gabola’, amesema kuwa ameongozwa na maandiko katika Biblia ambapo Yesu alibadilisha maji kuwa divai.

“Watu wanao kunywa na kubatizwa na bia wana furaha na amani. Hii inamaanisha kuwa wanaishi katika kivuli cha Mungu,”amesema Askofu Tsietse

Aidha, Kanisa hilo lenye jina la ‘Gabola’ likimaanisha ‘Kunywa’ limesema kuwa linakubali kuwapokea waumini waliotoka makanisa mengine huku likiweka wazi kwamba idadi ya watu imeongezeka kufikia 500 ndani ya miezi miwili tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo.

Hata hivyo, Askofu huyo ameweka wazi kwamba ana mipango ya kuanzisha matawi ya kanisa lake hilo katika miji mbali mbali nchini Afrka ya Kusini, huku akiongeza kuwa waumini wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kadri siku zinavyokwenda.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 5, 2017
Mmarekani afikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujaribu kuipindua serikali