Mchungaji na mwanzilishi wa kanisa la Commonwealth la Zion Assembly (COZA) nchini Nigeria, Biodun Fatoyinbo ameshitakiwa kwa kesi ya ubakaji na binti aliyefahamika kwa jina la Busola Dakolo.

Ambapo kupitia mahojiano yaliyofanywa na chombo cha habari cha YNaija binti huyo alifunguka kwa kina namna ambavyo mchungaji huyo alifanikisha tukio la kumbaka akiwa nyumbani kwa binti huyo ambaye familia yake ilikuwa wafuasi na washiriki wazuri wa kanisa lake.

Kufutia shutuma hiyo, mchungaji Biodun Fatoyinbo ametumia mtandao wake wa Instagram kutangaza kuachia kwa muda wadhifa wake wa uchungaji katika kanisa la COZA.

Mrs Dakolo, ambaye ni mke wa mwanamuziki, Timi Dakolo amekiambia chombo cha habari cha YNaija kuwa alikuwa mwenye umri wa miaka 16 pindi Fatoyinbo alipokuja nyumbani kwao Ilorin na kumbaka mara mbili ndani ya wiki moja.

Mrs Dakolo, ambaye kwa sasa ni mama wa watoto watatu amesema tukio la kwanza lilitokea asubuhi kipindi ambapo Fatoyinba aligonga mlango wa nyumabni kwao Ilorin.

”Haraka nilifungua mlango, alinisukuma, hakusema kitu wala kutamka neno lolote, alinisukumia tu kwenye kiti chumbani kwangu” akihadithia Mrs Dakolo.

”Nilimuona akitoa mkanda wake, na kuniambia kaa kimya, fanya nachotaka wewe ufanye na utakuwa salama,”aliongezea Mrs Dakolo.

Mrs Dakolo aliongezea kuwa mchungaji huo mara baada ya kukamilisha hitaji lake alimwambie amshukuru Mungu kwa kuwa kitendo hiko kimefanywa na mtu wa Mungu.

Mrs Dakolo akihadithia tukio hilo anasema amebeba mzigo huo moyoni kwa muda wa miaka saba hadi sasa anamshukuru Mungu kwa kupata ujasiri wa kuzungumza hadharani

Aidha, Mchungaji huyo amepinga shutuma hizo na polisi wanasema hawakupata malalamiko yeyote kutoka kwa Bi Dokolo na hakuna mtu aliyekwenda polisi kutoa malalamiko ya ubakaji dhidi ya mchungaji huyo.

Hata hivyo imemlazimu kuachia wadhifa wake kutokana na kashfa hiyo

Video: Hawa ndio viumbe wanaoishi muda mrefu na mfupi zaidi duniani
Rapa 50 Cent amkana mwanae hadharani