Mchungaji wa Kanisa la Mount Zion General Assembly la Afrika Kusini aliyetajwa kwa jina la Lethebo Rabalango, amedaiwa kumtoa uhai muumini wake wa kike katika harakati za kutaka kuonesha muujiza.

Mchungaji huyo anadaiwa kumkalizia muumini huyo Spika nzito iliyokuwa kanisani hapo na baadae yeye mwenyewe kukaa juu ya spika hiyo, akitaka kuwaonesha waumini kuwa kama Yesu alitembea juu ya maji hata yeye kwa uwezo wa Mungu anaweza kufanya lolote.

Kwa mujibu wa ‘the Southern Daily’ ya Afrika Kusini, mchungaji huyo aliita kikundi cha sifa na maombi mbele, na kisha akamwambia mwanamke huyo alale chini kabla ya kumkalizia spika nzito na yeye kukaa juu yake.

Spika 2

Hata hivyo, muujiza huo ulishindwa kutimia na waumini walimshuhudia msichana huyo akiwa kimya ndani ya dakika tano.

Imeelezwa kuwa baada ya mchungaji huyo kuwataka waondoe spika juu yake, msichana huyo alikuwa tayari amezimia na viongozi wengine wa kanisa walimpa huduma ya kwanza na baadae kumkimbiza hospitalini.

Vipimo vya madaktari vilionesha kuwa alikuwa amevunjika sehemu ya mbavu zake na baadae alifariki dunia kutokana na maumivu ya ndani ya mwili.

Katika hali ya kushangaza, mchungaji huyo alimlaumu msichana huyo aliyefariki akidai kuwa alikuwa na imani ndogo kiasi cha kushindwa kuhimili jaribio dogo.

Waliovuliwa Uanachama Young Africans Wakimbilia TFF
Utafiti: Kuangalia TV kupita kiasi hupunguza uwezo wa kuzalisha mbegu za kiume