Mchungaji wa kanisa la Grace and Power Prophetic Ministry International huko nchini Nigeria, David Elijah amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa njiani kuelekea kanisani.

Mchungaji Elijah ni miongoni mwa wachungaji vijana na tajiri nchini Nigeria.

Ijumaa ya Septemba 7, 2018 akiwa mjini Awka, Anambra huko Nigeria kwenye gari yake akielekea kanisani kwake alivamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto na kuanza kumfyatulia risasi.

Nusu ya gari hilo lilitobolewa kwa risasi maaskari walifika eneo la tukio na kumkuta mchungaji David Fulana yake ikiwa yenye matundu ya risasi huku mwili wake ukiwa haujajeruhiwa hata kidogo.

Hata hivyo, maaskari hao walimkamata kwa mahojiano zaidi huku wakitahamaki tukio hilo kwamba amewezaje kupona kwenye shambulizi hilo.

Tayari Jeshi la Polisi katika jimbo la Anambra limemuachia Mchungaji huyo siku ya Jumamosi baada ya kujiridhisha kuwa mtu huyo alikuwa salama na ni raia mwema.

Mchungaji David anatajwa kuwa moja ya wachungaji vijana wenye utajiri Mkubwa nchini Nigeria. Baada ya tukio hilo la kushambuliwa jana David alionekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa ameshika maburungutu ya fedha huku akiweka Captions kuwa yupo nchini Malaysia kikazi.

Maoni mengi ya wadau mitandaoni nchini Nigeria yanaonekana kushangazwa na tukio hilo, huku wengi wao wakidai kuwa Mchungaji huyo anatumia nguvu za giza.

Video: Marais wa Afrika waliopunguza mishahara yao
Icardi, Dybala kuongeza nguvu dhidi ya Colombia