Mchungaji maarufu nchini Kenya, James Ng’ang’a wa Kanisa la Neno Evangelist Ministry ametishia kufunga matawi ya kanisa lake la Neno Evangelism kwa madai kuwa Maaskofu hawamheshimu mke wake.

Katika kanda ya video iliyosambaa katika vyombo vya habari, ameonekana akiwakaripia maaskofu kwamba atawafukuza wote iwapo hawataheshimu onyo lake akidai kuwa matawi hayo yamekuwa vibanda na sio makanisa.

”Wakati huu nitawaonyesha uwezo wangu, mwanamke yeyote ambaye hatamuheshimu mke wangu, mlinikuta hapa na wake zenu, mmejitajirisha kupitia juhudi zangu, Wajinga nyie, Wajeuri, nilikuwa nikihubiri katika mikokoteni mpaka hapa nilipofikia, naapa mbele ya Mungu nitawaonyesha Ng’ang’a ni nani,”amesema Ng’ang’a

Aidha, amewaonya kwamba kama hawatamheshimu yeye na mke wake atawafukuza katika kanisa lake bila kujari vyeo walivyo navyo hivyo wanatakiwa kuwa makini muda wote hasa kumheshimu mke wake.

Amesema kuwa kwasasa amefikia umri wa kuheshimiwa na maaskofu hao wa kanisa lake na kila anapo kohoa ni lazima watii kwasababu anakabiliwa na changamoto ya shetani anataka kuliangusha kanisa lake.

Ng’ang’a amewaita maaskofu wake kuwa watu wasio na maana, wajinga na wasiomuheshimu kama mtu aliyewasaidia mpaka kupata utajiri walioupata mpaka sasa.

Bangi yamponza, asukumwa ndani miaka 30
Video: MO Dewji afunguka kutekwa kwake, Takukuru yanusa maficho ya bilionea

Comments

comments