Waumini wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God jijini Dar es Salaam jana waliadhimisha Sikukuu ya Pasaka ambayo ni kumbukumbu ya kufufuka kwa Mkombozi wao Yesu Kristo, huku wakiondoka na ujumbe wa amani na matumaini katika maisha yao.

Katika mahubiri na salamu zake za Pasaka, Mchungaji Dkt. Getrude Lwakatare amewasihi watanzania kupendana na kudumisha amani, huku wakiamini kuwa kifo na hatimaye kufufuka kwa Yesu Kristo, ni ishara tosha kwamba mwisho wa matatizo yanayomkabili kila mtu katika maisha yake umekaribia.

Aidha, Dkt Lwakatare amesema kuwa kama ilivyotokea kwa Yesu Kristo, watanzania na hususani waumini wa dini ya Kikristo wanapaswa kuwa na imani kuwa matatizo pamoja na shida mbali mbali zinazowakabili mwisho wake umekaribia.

Chadema: Hatutawajibika kwa chochote kuhusu Afya ya Mdee
Video: Viongozi Chadema wahamia Gerezani, Nyundo za Maaskofu Zaitesa Serikali

Comments

comments