Wakati zoezi la bomoabomoa likiendelea katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam bila ‘simile’ kwa yeyote aliyewekewa alama ya X, mchungaji wa kanisa la Assemblies of God lililoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, Dk. Getrude Lwakatare amepinga jumba lake la kifahari liliko Mikocheni kubomolewa baada ya kuwekewa alama ya X.

Jumba hilo liliwekewa alama hiyo ya ‘X’ hivi karibui na wizara ya Maliasili na Utalii kupitia wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na madai kuwa liko katika eneo la hifadhi ya ufukwe wa bahari.

Nyumba

Akizungumza jana na waandishi wa habari kwa niaba ya mchungaji Lwakatare, Mwanasheria wake ambaye ni wakili wa kujitegemea kutoka katika kampuni ya Msekwa & Company Advocates, Jerome Msemwa aliitaka serikali kutobomoa jumba hilo na kuheshu uamuzi wa mahakama kuu kwa kuwa ilishatoa hukuku na kuonesha kuwa mteja wake hakukiuka taratibu zozote za ujenzi.

“Jengo la mteja wangu limewekewa alama X ili libomolewe. Lakini ujenzi wa nyumba hiyo ulishajadiliwa na kesi yake kuhukumiwa na Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi na akaonekana hakuvunja taratibu zozote za ujenzi. Hukumu ilitolewa Mei 22 mwaka jana na nakala ipo,” alisema Msekwa.

“Ubomoaji huo ni batili na tunaziomba mamlaka zote zinazhohusika kuheshimu hukumu iliyotolewa, na endapo utekelezaji huo utafanywa itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki,” aliongeza.

Alisema kuwa nyumba ya mteja wake ina thamani kubwa na endapo itabomolewa mteja wake hana sehemu nyingine ya kwenda na kwamba kufanya hivyo utakuwa kukiuka sheria na haki.

CCM wamshukia Lowassa kuhusu wafanyabiashara na Kodi
Wananchi wagawana shamba la Sumaye, mwenyewe anena