Mchungaji  maarufu kwa jina la Rufus Phala kutoka kanisa la AK Spiritual Christian lililopo Makgodu, Limpopo, Afrika Kusini amewashangaza watu kwa kitendo cha kuwanywesha  Dettol waumini wake ilihali ina madhara kwa binadamu.

Kwa mujibu wa Daily Sun SA, mchungaji huyo alifanya kitendo hicho kwenye ibada za kawaida kanisani kwake akiwataka waumini wenye matatizo na wanaohitaji maombi wanywe Dettol aliyokuwa ameishika mkononi mwake huku akiwaambia watapona shida zao ikiwemo magonjwa.

“Nafahamu kuwa Dettol ni sumu, lakini Mungu ameniagiza niwape na muitumie. Mimi nilikuwa wa kwanza kuinywa,”  – Mchungaji.

Pia amesema kuwa amepokea meseji za WhatsApp kutoka kwa watu waliokunywa na wamethibitisha kupona.

Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, amehojiwa Daktari kutoka Afrika Kusini, Dr Mabowa Makhomisane, ambaye amekiri kuwa Dettol ina madhara inapotumika tofauti na maelekezo ikiwemo kuinywa

“Mtu akinywa Dettol na ikafika tumboni, kimsingi hupunguza mzunguko wa hewa ya Oxygen mwilini, hali hiyo ikitokea mtu anaweza kupoteza fahamu na kufariki, na kama mtu atatapika na bahatihttp://dar24.com/wp-admin/post-new.phpN mbaya maji maji yakaingia kwenye mapafu yake, Detto itamsababishia ugonjwa wa Nimonia, mapafu yatajikunja na mtu atashindwa kupumua”

Dr Makhomisane amewashauri watu waliokunywa dawa hizo waende Hospitali kupata vipimo ili kujua madhara waliyopata.

Magufuli aanza mchakato wa kuwanyoosha wafuasi wa Lowassa CCM
Lowassa, Mnyika Kusimamia uchaguzi Tabora