Mchungaji wa kanisa la Mikocheni B Assemblies of God,  Dr Getrude Rwakatare amewatoa wafungwa 12 waliokuwa wamefungwa kwenye gereza la Keko jijini Dar es Salaam huku lengo ni kuwarejesha uraiani wafungwa 78 walioko jela kwa kukosa kulipa faini ndogo ndogo.

Akizungumza na waandishi wa habari Rwakatare alisema kuwa amewatoa wafungwa wanaodaiwa kiasi kidogo cha fedha na wenye makosa madogo madogo ili waweze kurejea uraiani na kujenga taifa kwani kuendelea kuishi huko wanapoteza nguvu kazi ya kesho.

“Nipo gereza la Keko ambapo nina furaha kuwatoa wafungwa ambao wamefungwa mahali hapa kwasababu mbalimbali. Wengine wameshindwa faini ya shilingi elfu 40, wengine wameshindwa faini ya shilingi elfu 50 na wengine kukosa faini za laki moja,” alisema mchungaji Rwakatale

Baada ya Keko, Mama Rwakatare ataelekea katika gereza la Ukonga kwa ajili ya kuendelea na shughuli hiyo na amesema kuwa ametenga kiasi cha shilingi milioni25 kwaajiri ya kuwatoa wafungwa hao na aliongeza kuwa yeye kama mtumishi wa mungu ameguswa kufanya hivyo.

Umoja wa Mataifa Kuiwekea Korea Kaskazini Vikwazo
Mourinho Azidi Kuhaha Kuelekea Mchezo wa Derby,Mchezo Kati ya Manchester United na Manchester City