Mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es salaam, Halima Mdee amesema kuwa hajaenda kuripoti kwa DCI kama ilivyotakiwa kwa sababu yeye hajapatiwa wito rsmi wa kufika katika ofisi hizo kwaajili ya mahojiano.

Amesema kuwa mpaka sasa hajapata barua yeyote kutoka kwa DCI kwani ametoa tangazo la ujumla, lakini yeye binafsi hajapewa wito wowote, hivyo hawezi kwenda kutokana na taarifa hiyo.

“Mimi nimesikia tangazo la ujumla, wakiniita in personel Halima njoo nitaenda na hakuna popote kwenye kauli yao iliposema Halima Mdee njoo, lakini siwezi kwenda kwa ‘general statement’, amesema Mdee

Hata hivyo, Juzi Jeshi la Polisi liliwataka watu wote waliopost kwenye mitandao ya kijamii kuhusu askari wao aliyepo jijini Nairobi wakimuhusisha na kumfuatilia, Tundu Lissu nchini Kenya kwenye matibabu kutakiwa kuripoti wenyewe kwa DCI, kabla ya kitengo cha sheria za makosa ya mtandaoni hakijawachukulia hatua zaidi.

 

Mbunge wa CCM aliyemkodia ndege Lissu atoboa siri
Isco kubaki Santiago Bernabeu mpaka 2022