Sakata la Mbunge wa Jimbo la Kawe lililopo jijini Dar es salaam, Halima Mdee limeendelea kuwa gumzo mara baada ya kuendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku kadhaa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi.

Katika sakata hilo, Mdee anashikiliwa na jeshi la polisi huku jeshi hilo likishindwa kuweka wazi ataachiliwa huru ama kufikishwa mahakamani licha ya masaa 48 yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kumalizika.

Aidha, Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha) alikamatwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi ambayo yangeweza kusababisha kuhatarisha amani.

Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene amesema kuwa mpaka sasa hawaelewi kinacho sababisha mbunge huyo kuendelea kushikiliwa na jeshi la polisi.

?LIVE: Rais Dkt. Magufuli akipokea nyumba 50 kutoka taasisi ya Mkapa
Alikiba Ft Davido 'Coming soon'