Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Njombe Mji na Simba SC uliokuwa uchezwe tarehe 11, Machi 2018 katika dimba la Sabasaba mjini Njombe, umeondolewa.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB), Boniface Wambura imesema kuwa mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine.

Katika taarifa hiyo Wambura ameeleza kuwa sababu ya mabadiliko hayo ni kuipa nafasi Timu ya Simba SC kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, utakaochezwa tarehe 17, Machi 2018 nchini Misri.

Florida wapitisha muswada wa usalama shuleni
Ummy Mwalimu awaonya wakurugenzi wote nchini