Mshambuliaji Wa Kimataifa wa Rwanda Meddie Kagere ametoa mtanzamo wake juu ya hoja ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupunguza wachezaji wa kigeni.

Kagere ambaye ni mshambuliaji wa kutumainiwa kwenye kikosi cha mabingwa wa Tanzania bara Simba SC, amekuwa na kiwango bora katika ligi ya VPL tangu aliposajiliwa miaka miwili iliyopita akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa yupo nchini kwo Rwanda, ametoa maoni tofauti dhidi ya hoja ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupunguza wachezaji wa kigeni.

Amesema uwepo wa wachezaji wengi wa kigeni katika ligi ya Tanzania bara ama ligi nyingine yoyote duniani, kuna faida kubwa hasa linapokua suala la ushindani kwenye kikosi cha klabu moja na kisha klabu na klabu.

Amesema suala kubwa katika hoja hiyo ni kuhakikisha kunakuwa na wachezaji wengi wa kigeni wenye ubora, ambao utaendelea kutoa chachu kwa wachezaji wazawa.

“Uwepo wa wachezaji wengi wazuri wa kigeni katika ligi fulani unaongeza chachu ya ligi hiyo kupiga hatua kwa maana kuwa na ushindani na hata Klabu zake kufanya vizuri Katika mashindano ya Kimataifa kwa Hilo lazima liangaliwe Vizuri kabla halija tolewa maamzi.”

“Hoja hii kwangu mimi ninaona izingatie ubora wa wachezaji wanaosajiliwa na sio idadi, kupungua kwa idadi ya wachezaji wa kigeni hakutoleta tija ya ushindani, lakini kigezo cha ubora wa wachezaji ndio kitakua na thamani zaidi ya kuendelea kukuza ushindani kwa wachezaji wazawa.” Alisema Kagere.

Chelsea kufuata nyayo za Arsenal, West Ham Utd
Luc Eymael kusajili saba young Africans