Mshambuliaji wa timu ya Simba Sc, Meddie Kagere huenda akaihama timu hiyo na kutimkia nchini Marekani kwenda kusakata kabumbu baada ya kuandaliwa ofa ya uhamisho na wakala wake Patrick Gakumba.

Gakumba amesema kwa kasi aliyonayo tayari ameshamuandalia ofa  katika klabu ya Dallas FC iliyopo Texas, Marekani ili mchezaji huyo aweze kwenda kucheza soka.
Gakumba amesema moja kati ya masharti ambayo Dallas wanayataka ili Kagere wamchukue ni kuhakikisha anafikisha mabao 25 msimu huu kunako ligi kuu bara,
“Najua kwa sasa Kagere ni mali ya Simba, nawasiliana naye nikimtaka azidi kuitumikia klabu hiyo kwa nguvu zote huku akikumbuka deni la mabao 25 linalohitajika.
”Dau la kule litakuwa ni nono zaidi ya Msimbazi, na tayari jina lake limeshajulikana katika nchi nyingi za Afrika na duniani kwa ujumla.”
Mpaka sasa Kagere aliyecheza mechi nne msimu huu amefunga magoli sita huku mchezaji mwenzie anaye mfuatia katika timu yake ya Simba kwa ufungaji wa mabao ni Miraji Athumani mwenye mabao matatu na msimu uliopita Kagere alifunga magoli 23.
Ziara ya Majaliwa Itigi, Vigogo watakiwa 'kutapika' pesa za Serikali
JPM ampongeza RC Chalamila kuwachapa wanafunzi, awakaanga wanaokosoa