Wapinzani wa Young Africans katika Michuano ya Kombe la Shirikisho la barani Afrika, Medeama S.C. ya Ghana wamebadili mfumo wa kuwasili nchini.

Awali Medeama walitarajiwa kufika mapema leo asubini lakini kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuwekwa wazi, wawakilishi hao pekee wa Ghana katika michuano ya kimataifa watawasili mchana wa leo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Alfred Lucas, wakali hao kutoka Ghana watawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere kwa Shirikia la Ndege la Kenya Airways (KQ) mchana wa leo, huku wakiwasili kimafungu-mafungu.

Gadner Afunguka Kuhusu Kumdhalilisha Jide Mitandaoni
Tanzania Yachupa Kwa Nafasi 13 Duniani