Kocha Mkuu wa Coastal Union Melis Medo ameionya Young Africans kwa kusema isitegemee matokeo mazuri kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa mwishoni mwa juma hili (Jumapili-Januari 16).

Young Africans haijawahi kupata ushindi kwa misimu kadhaa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwanui kwa misimu kadhaa, hali ambayo inaendelea kunogesha pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.

Kocha huyo kutoka nchini Marekani amesema mchezo huo utakua mgumu, lakini lengo kubwa kwao ni kuhakikisha wanafanya vizuri na kupata alama tatu muhimu kwenye uwanja wao wa nyumbani.

“Mchezo utakuwa nzuri na mgumu. Siyo siri kuwa Young Africans msimu huu ni nzuri na ina wachezaji wazuri, lakini ikumbukwe msimu uliopita walifungwa hapa. Kwa hiyo na sisi msimu huu tuna timu nzuri kuliko hata msimu uliopita, waje vizuri tu,” amesema Medo.

Amesema hawataweza kukubali kufungwa kirahisi kwa sababu walipoteza mchezo uliyopita nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar, hivyo hawawezi kuruhusu kupoteza tena.

Desemba 28, mwaka jana, Coastal ilichapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani bao 1-0 na Mtibwa Sugar.

Young Africans haijaifunga Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani kwa misimu saba mfululizo.

Mara ya mwisho Young Africans kupata ushindi kwenye uwanja huo, ilikuwa ni Februari 4, 2015 (Msimu wa 2014/15), iliposhinda 1-0 lililofungwa na nahodha na beki wao mahiri kwa wakati huo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 11 ya mchezo.

Chama kuvaa 17, Sakho namba 10
Simba SC, RS Berkane mambo safi