Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump anatarajia kufanya ziara ya nchi nne barani Afrika, mwezi Oktoba mwaka huu.

Ziara hiyo itakayo anza Oktoba mosi, Melania anatarajia kuzitembelea nchi za Ghana, Malawi, Misri na Kenya

Amezitaja nchi anazotarajia kuzitembelea katika mkutano wake na Wake wa marais wanao hudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York.

Amesema kuwa nchi hizo zimechaguliwa azitembelee kwasababu zimekuwa zikifanyakazi bega kwa bega na Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID).

Katika mkutano huo, Melania Trump alitambua uwepo wa mke wa rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Margareth Kenyatta na kusema kuwa ilikuwa ni heshima kubwa kumpokea White House.

“Huko Kenya, USAID inafanya kazi kwa kushirikiana katika programu mbalimbali, ikiwemo ya elimu ya awali ya watoto, kuhifadhi mazingira ya wanyama pori na kujikinga na Virusi vya Ukimwi,” amesema Melania Trump

Hata hivyo, ameongeza kuwa shirika la USAID linafanyakazi pia katika nchi za Ghana, Malawi na Misri katika huduma za afya na inasaidia juhudi zinazoendelea kupanua huduma hizo na ubora wake kwa mama na mtoto mchanga anayezaliwa, na kuwaelimisha kina mama na watoto wadogo juu ya umuhimu wa lishe bora.

 

Breaking News: Rais Magufuli akizindua Flyover muda huu
Video: Waliofariki ajali ya MV Nyerere wafikia 228, JPM kuandika historia mpya leo