Meli ya Kijeshi ya Marekani imepata ajali katika Bahari ya Japan mara baada ya kugongana na Meli ya mizigo kutoka nchini Ufilipino.

Meli hiyo ya kijasusi ya kutungua silaha za nyuklia kutoka Marekani bado haijajulikana ni wapi ilipokuwa ikielekea kwa wakati huo.

Aidha, kwa taarifa zilizotolewa na msemaji wa Jeshi la Marekani zimesema kuwa mabaharia saba waliokuwemo katika Meli hiyo wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali hiyo.

Hata hivyo, Meli ya mizigo ACX Crystal ilikuwa ikifanya safari zake katika miji ya Nagoya na Tokyo nchini Japan kwaajii ya kusafirisha mizigo.

Urusi yaikung'uta New Zealand goli 2-0
Video: Sumaye, Warioba wakoleza moto makinikia ya Acacia, Hakuna kama JPM Afrika