Meli kubwa ya mizigo yenye urefu wa mita 150 kutoka nchini Urusi,  imewasili na kutia nanga kwenye bandari ya Tanga, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 300.

Meli kubwa ya mizigo toka nchini Urusi.

Meneja wa Bandari Tanga, Masoud Mrisha amesema Meli hiyo imebeba shehena ya mbolea kwa ajili ya viwanda vya madini,  na ujio wake ni matunda ya uwekezaji uliofanywa na Serikali.

Meneja wa Bandari Tanga, Masoud Mrisha

Amesema Meli hiyo imebeba mzigo wa tani 6909, unaopelekwa  nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC na utaanza kushushwa  hii leo Februari 27 -28, 2023.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 28, 2023
Uongozi ni kuwatumikia Wananchi: Dkt. Mwinyi