Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ACT Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa 2020, Benard Membe amesema yuko njiani kurudi mahali fulani ambapo hakupataja, huku akisema anasubiri uamuzi wa shauri lake lililoko mahakamani hapo Oktoba 12 mwaka huu.

Akiwa kwenye mkutano wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Membe alisema anamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na yupo tayari kumpigia kampeni katika Uchaguzi Mkuu 2025.

“Niwaombe tusahau yaliyopita kuanze upya tujenge rondo na taifa letu Niko tayari kuwa kampeni meneja wake rais uchaguzi mkuu mwaka 2025,” amesema Membe.

Aidha amesema kuwa wakati wote yuko tayari yeye na wananchi wa Rondo kumpa ushirikiano Rais na serikali yake kwa kuwa ameonyesha dhamira ya kuirudisha nchi kwenye misingi ya umoja, mshikamano na mahusiano ya kitaifa na kimataifa.

Amemuomba Waziri Mkuu Majaliwa kufikisha salamu na pongezi kwa Rais samia suluhu kwa kazi mzuri anayofanya.

Kwa upande wake Waziri Wkuu Majaliwa amesema amezipokea pongezi hizo kwa niaba ya rais na atazifikisha kwa raisi na kuwaomba wananchi wa Rondo kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya afya, elimu, mbiundombinu.

Unyanyasaji wa kingono Ufaransa wamsikitisha Papa Francis
Habari kubwa kwenye Magazeti leo, Oktoba 6, 2021