Mshambuliaji wa Man Utd Memphis Depay usiku wa kuamkia hii leo aliisaidia timu yake ya taifa kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Luxembourg katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

Mshambuliaji huyo ambaye alitua Old Trafford kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 25 akitokea  PSV mwaka 2015, alifunga mabao mawili katika mchezo huo huku bao lingine la Uholanzi likifungwa na Arjen Robben.

Bao la wenyeji Luxembourg lilifungwa kwa njia ya mkwaju wa penati na Maxime Chanot.

Ushindi huo umeiwezesha Uholanzi kufikisha point saba katika msimamo wa kundi la kwanza na wanashika nafasi ya pili, wakitanguliwa na mabingwa wa dunia mwaka 1998 timu ya taifa ya Ufaransa.

Michezo mingine ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2018 iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo kanda ya bara la Ulaya ni:

Kundi A

Bulgaria1 – 0 Belarus

Luxembourg 1 – 3 Uholanzi

Kundi B

Hungary 4 – 0 Andorra

Switzerland 2 – 0 Visiwa vya Faroe

Ureno 4 – 1Latvia

Kundi H

Cyprus 3 – 1 Gibraltar

Ublegiji 8 – 1 Estonia

Ugiriki 1 – 1 Bosnia-Herzegovina

Harry Kane Kuikosa Hispania
Mohamed Salah, Abdallah Saied Waizima Ghana