Società Sportiva Calcio Napoli wanajiandaa kuwasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Man Utd Memphis Depay wakati wa dirisha dogo la usajili.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, anakabiliwa na changamoto ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Man Utd tangu alipowasili meneja Jose Mourinho mwezi Julai mwaka huu.

Hata hivyo taarifa kutoka Old Trafford zinaeleza kuwa, Mourinho yupo tayari kumuachia Depay, lakini kwa masharti ya usajili wa mkopo kutokana na mustakabali wa kikosi chake kwa sasa, ambao hauonyesha kama kitakua na ushindani wa dhati katika kuwania ubingwa wa ligi ya England msimu huu.

Società Sportiva Calcio Napoli wanaamini kama watafanikiwa kumsajili Depay, watakuwa wamekamilisha azma ya kusuka vyema safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inaendelea kuhangaika baada ya kuondoka kwa Gonzalo Gerardo Higuaín.

Wakati mipango ya klabu hiyo ya kusini mashariki mwa Italia ikipangwa, huenda upinzani wa usajili wa Depay ukaibuka kutokana na klabu nyingine za Italia kama AC Milan na AS Roma kutajwa kuiwania saini yake.

Mbali na klabu hizo za Italia, pia klabu ya zamani ya mshambuliaji huyo PSV Eindhoven nayo imeonyesha nia ya kumsajili.

Trump apiga teke bakuli la ‘mshahara wa Urais’
Luis Suarez Ampigania Glen Johnson FC Barcelona