Baada ya kung’ara katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, akiwa na timu yake ya taifa ya Uholanzi mshambuliaji Memphis Depay, ameshindwa kutoa kauli ya mustakabali wake ndani ya kikosi Man Utd.

Mshambuliaji huyo alifunga mabao mawili kati ya matatu yaliyoipa ushindi timu ya taifa ya Uholanzi katika mchezo dhidi ya Luxembourg usiku wa kuamkia hii leo.

Baada ya mchezo huo kumalizika Depay alihojiwa na waandishi wa habari na aliulizwa kuhusu mustakabali wake ndani ya kikosi cha Jose Mourinho, alijibu bado hajafahamu nini kinachoendelea lakini angependa kubaki Old Trafford.

“Sifahamu chochote kuhusu mustakabali wangu, lakini natambua bado nina umuhimu Man Utd.

“Ningependa kuendelea kubaki kwa sababu ninapendezwa na mazingira na ushirikiano uliopo baina yangu na wachezaji wengine, japo ninakabiliwa na changamoto ya kutokucheza mara kwa mara. Alisema Depay

Tayari baadhi ya klabu za barani Ulaya zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wakati wa dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa rasmi mwezi Januari mwaka 2017.

Awali klabu za SSC Napoli, AC Milan na AS Roma zote za Italia zilitajwa kumuwania Dapay, huku klabu ya PSV Eindhoven iliyokubali kumuachia mwaka 2015 ikiwa miongoni mwa wanaoiwania saini yake.

Nchini England taarifa zinaeleeza kuwa meneja wa klabu ya Everton Ronald Koeman, naye anatamani kumsajili Depay kutokana na kumfahamu vyema uwezo wake wa kusakata kabumbu.

Video: Tetemeko kubwa latokea New Zealand
Harry Kane Kuikosa Hispania