Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu, Glory Mziray amefariki dunia jana majira ya mchana akiwa ofisini kwake jengo la Mpingo wakati akifanya mkutano na waandishi wa habari juu ya kupandishwa hadhi kwa misitu 7.

Meneja huyo alishikwa na umauti wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari yaliyotokana na kile alichokuwa akiwasilisha.

Hapa ndipo ule msemo usemao hakuna ajuaye siku wala saa unavyotimia kwa meneja huyu kijana, ambaye dakika chache zilizopita hakuwa mgonjwa wala hakuonesha kupata shida yeyote kwani alijiandaa vyema kuiwakilisha wizara yake.

Glory alikutwa na mauti mara baada ya mmoja ya mwandishi wa habari kumtaka ajitambulishe kwa majina na cheo chake kwani hakufanya hivyo mwanzoni wakati akitoa hotuba yake.

Ambapo dakika kadhaa baada ya kusimama kujibu swali hilo, Glory alianza kubadilika gafla na kuanza kupoteza sauti na kupoteza fahamu kabisa.

Wanahabari walimpa huduma ya kwanza bila mafanikio, ndipo wakaamua kumkimbiza hospitali ya TMJ chang’ombe ambapo madaktari walimfanyia uchunguzi na kubaini kuwa alipoteza maisha kabla ya kufika hospitali hapo.

Aidha, Daktari Chris Peterson ameeleza kuwa familia yake imesema Glory alikuwa na tatizo la Shinikizo la damu.

 

 

Aliyekamatwa akimtorosha mwanaye hospitalini kukwepa bili aneemeshwa
Matawi ya CUF yavamiwa usiku wa manane