QBaada ya kuripotiwa amejiunga na Mabingwa Ligu Kuu ya Wanawake Simba Queens, Meneja wa mchezaji Irene Kisisa, ametangaza kuachana na Mchezaji huyo.

Irene amejiunga na Simba Queens akitokea klabu ya Yanga princess ambayo ilimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Ya Wanawake msimu huu 2020/21.

Inadaiwa kuwa mchezaji huyo amefanya maamuzi ya kujiunga na Simba Queens bila kumshirikisha meneja wake.

Hatua hiyo imemkasirisha George Job ambaye ni meneja wa Irene, na ametangaza kupitia taarifa maalum alioisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Taarufa ya George Job inasomeka: “Baada ya kufanya kazi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja na Mchezaji Irene Kisisa ‘Rodrygo’ kama msimamizi wake kwenye masuala ya michezo leo tarehe 23, 06, 2021 nimeamua kusitisha mahusiano hayo rasmi”

“Hivyo basi mimi George Job sihusiki tena na masuala yoyote yale yanayohusiana na Mchezaji huyo”

“Namtakia kila la kheri kwenye maendeleo yake ya soka”

Yanga, TFF mambo safi
Hii ndo suluhu ukatili dhidi ya watoto