Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Awamu ya Nne, Benard Membe amesema kuwa alikuwa karibu sana na marehemu Dkt. Reginald Mengi .

Amesema kuwa amepoteza mtu aliyekuwa rafiki mkubwa wa familia yake kwa zaidi ya miaka 12 ambapo amesema kuwa walikuwa wakishauliana katika masuala mbalimbali ya kibiashara na uchumi.

Ameyasema hayo mkoani Kilimanjaro wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa marehemu Dkt. Reginald Mengi ambapo amesema kuwa Mengi alishirikiana sana na serikali wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa chini ya Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

”Katika harakati zangu za kuwania kugombea Urais, Dkt. Mengi aliniunga mkono mwaka 2015, niseme tu kwamba mzee Mengi hakuwa mbaguzi kwa mtu yeyote aliyekuwa na nia ya kugombea Urais, wote aliwasaidia ingawa kuna wengine walikataa na mimi namkubali sana,”amesema Benard Membe

Hata hivyo, Membe amesema kuwa Dkt. Mengi alishirikiana kwa ukaribu mkubwa na serikali ya Awamu ya Nne kipindi ambacho yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

LIVE: Mazishi ya Dkt. Reginald Mengi Machame - Kilimanjaro
Mzee Mengi hakuwa mbaguzi kwa wanasiasa- Nape Nnauye

Comments

comments