Msanii wa Bongo fleva, MC, na Muigizaji wa filamu nchini, Menina Abdulkarim hatimaye ameitikia wito na kufika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) zilizopo Sharif Shamba, Ilala jijini Dar Es Salaam ili kutoa maelezo yake juu ya kusambaa kwa video na picha zake za utupu kupitia mitandao ya kijamii.

Kupitia mahojiano kati ya msanii na BASATA kwa pamoja wamesikiliza maelezo ya Msanii Menina Abdulkarim na nini kilichojitokeza katika sakata zima la kusambaa kwa video na picha zake za utupu kupitia mitandao ya kijamii.

Ambapo BASATA imesema Kwa kuwa suala la kusambaa video na picha za utupu za Msanii Menina katika mitandao ya kijamii lipo mikononi mwa mamlaka nyingine, imeamua kuyafanyia kazi maelezo yake.

Taarifa hiyo imetolewa na Godfrey L.Mngereza Katibu Mtendaji-BASATA.

Aidha, mara kadhaa BASATA kupitia utaratibu wake wa kutoa Elimu kwa wasanii na Umma wamekuwa wakiwaelekeza wasanii wote kote nchini kufanya kazi zao za Sanaa kwa kuzingatika maadali mema kwa jamii,pamoja na kufuata taratibu za kujisajili,lakini kwa bahati mbaya baadhi ya wasanii wamekuwa hawazingatii maelekezo hayo na hivyo kujikuta wanavunja sheria za nchi.

Video: Tazama ngoma mpya ya Vanessa aliyomshirikisha Rayvanny, 'Bado'
Watoto 550,388 kupatiwa chanjo Dodoma