Baba wa mtoto kutoka nchini Afghanistan, Murtaza Ahmadi amelazimika kuihamishia familia yake nchini Pakistani, kufuatia vitisho ambavyo wamekua wakivipokea kutoka kwa watu wasiojulikana baada ya mwanae kupewa zawadi na mshambuliaji wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Andres Leo Messi.

Baba wa mtoto huyu amesema siku kadhaa zilizopita alipokea simu nyingi kutoka kwa Wababe waliyedhani Messi katoa hela kwa Murtaza hivyo wanataka mgao wao, hiyo ni moja ya sababu zilizofanya wahame Afghanistan na kwenda kuishi Pakistan ambako Murtaza na wenzake saba wa familia hiyo wanaishi chumba kimoja.

1462266340081Mtoto Murtaza Ahmadi akiwa uwanjani kabla ya kupokea zawadi kutoka kwa Lionel Messi

Murtaza alionyesha kuwa na mapenzi ya dhati kwa Lionel Messi kwa kuvaa mfuko uliokua na mistari ya rangi ya bluu bahari na nyeupe na kisha aliiandika namba kumi na kuipa jina la mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa ndio mwanasoka bora wa dunia.

Messi aliopoiona picha hiyo aliingiwa na simanzi iliyochanganyika na furaha na alilazimika kumsaka kupitia kwa watu wake wa karibu, na alipompata alimkabidhi jezi mbili halisi ya timu ya taifa ya Argentina yenye namba kumi na iliyoandikwa jina lake.

Jezi hizo pia zilisainiwa na Lionel Messi kwa kuashiria ni zawadi halali kutoka kwake.

Ajira: Serikali yatangaza neema ya ajira mpya zaidi ya 71,000 ndani ya mwaka
Baraka Deusdedit: Fomu Kuanza Kutolewa Mei 27