Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2014 – 2015 wa ligi ya Hispania, La Liga katika hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika Jumatatu usiku.

Messi alimfunika mshindani wake mkuu wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo aliyeibeba tuzo hiyo mwaka uliopita.

Kutokana ushindi huo, Messi anakuwa na tuzo sita za La Liga kati ya miaka saba ya utoaji wa tuzo hizo ambapo ni tuzo moja pekee ya kipengele hicho iliyoenda kwa Ronaldo.

Messi pia alifanikiwa kubeba tuzo ya mshambuliaji bora wa mwaka wa ligi hiyo ambapo timu yake ilibeba tuzo tano usiku huo dhidi ya Real Madrid iliyobeba tuzo tatu.

Cristiano Ronaldo aliweza kubeba tuzo ya kukubalika na mashabiki wengi ‘fan voted price’.

 

Mchungaji aoa mpenzi aliyempa mimba, mkewe aibariki
Mbunge Afariki Akifanya Mapenzi Kwenye Gari