Washambuliaji wa Mabingwa wa Uhispania wanaotetea ndoo yao, Klabu ya Barcelona, Lionel Messi na Luis Suarez wanafanya mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mpango wa kumwaga wino wa kuongeza maisha ya soka katika klabu hiyo.

Kwa mujibu wa uongozi wa Barca, mpachika mabao kutoka Uruguay, Suarez anatarajia kumwaga wino wa kubaki Nou Camp hadi mwaka 2022.

Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu amesema kuwa taratibu zote za kimkataba zimekamilika na kwamba kilichobaki ni vitu vichache tu.

“Imekwisha, vimebaki vitu vichache avinavyopaswa kukamilishwa na tutawatangazia siku chache zijazo,” alisema Bartomeu.

“Tunamhitaji Luis Suarez aendelee kubaki katika Klabu kwa miaka mingi zaidi. Kwetu ni kiungo muhimu sana,” aliongeza.

Kwa upande wa Messi ambaye ameshashajikabidhi Barcelona hadi Juni 2018, Bosi wa  klabu hiyo, Luis Enrique amesema wanafuraha kubwa kwamba mazungumzo yanaendelea vizuri.

Suarez alishinda kiatu cha dhahabu cha Ulaya kinachotolewa kwa mpachika mabao mengi zaidi baada ya kupachika jumla ya magoli 40 katika Liki hiyo.

Mafiga matatu ya Barcelona yanayopika magoli mengi klabuni hapo, Messi, Suarez na Neymar yameshaivisha na kupakua jumla ya magoli 131 katika mashindano wakishinda kombe la La Liga na Copa del Rey.

 

 

Video: Dangote amhakikishia Rais Magufuli uwekezaji zaidi
Msaidizi wa Mbowe adaiwa kutoweka kiutata, Chadema na Polisi watofautiana