Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Arsenal ya England, Mesut Mustafa Ozil, yu mbioni kusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni laki mbili (200,000) kwa juma.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ana matumaini makubwa ya kukamilishwa kwa dili hilo, kutokana na fununu zinazoendelea kumuhusu Ozil kuhitajika kwenye klabu nguli za barani Ulaya kama Juventus pamoja na FC Bayern Munich.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, kwa sasa analipwa mshahara wa Pauni laki moja na arobaini (140,000) kwa juma, hivyo kutakua na ongezeko la Pauni elfu sitini (60,000) katika mshahara wake kama atakubalia kusaini mkataba mpya.

Arsene Wenger, pia anamuhangaikia, mshambuliaji wake kutoka nchini Chile, Alexis Sanchez ili aendelee kusalia klabuni hapo kwa kuwa mbioni kumsainisha mkataba mpya.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amekua katika ombwe la kuhusishwa na mipango wa kuihama The Gunners, baada ya kuchoshwa na mwenendo uliopo klabuni hapo wa kutofikia lengo la kutwaa ubingwa wa nchini England sambamba na kutofika mbali kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mbeya City Kumkosa Nahodha Wao Hassan Mwasapili J'pili
Mario Gotze Kucheza Soka Nchini England Msimu Ujao?