Kiungo wa klabu ya Arsenal Mesut Mustapher Ozil ametetea maamuzi ya kupiga picha ya pamoja na Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan, kwa kusema haina uhusiano wowote wa masuala ya kisiasa, zaidi ya heshima kwa kiongozi huyo.

Ozil alidhihirisha kupiga picha na Erdogan, baada ya kuianika katika mitandao ya kijamii, huku akielezea furaha ya kukutana na kiongozi huyo ambaye analiongoza taifa lenye asili ya wazazi wake.

Ozil, ambaye alikua sehemu ya kiosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2014, na kisha kuitwa tena kikosini kwa ajili ya fainali za mwaka huu 2018, alimtembelea Erdogan mwezi Mei, akiwa na mchezaji mwenzake Ilkay Gundogan ambaye ana asili ya Uturuki, wakati timu yao ya taifa ilipokuwa kambini kwa ajili ya kujiandaa na fainali za kombe la dunia zilizofanyika Urusi.

Wachezji hao walikutana na Erdogan jijini London- England ambapo kikosi cha Ujerumani kiliweka kambi kwa siku kadhaa, na ndipo Ozil alipopiga picha na kiongozi huyo.

Hata hivyo kuonekana kwa picha hiyo kulizua tafrani kwa mashabiki wa soka nchini Ujerumani ambao walihoji uhusiano wa mchezaji huyo na Erdogan, jambo ambalo Ozil amelipokea kama ubaguzi na kusababisha kutangaza kujiuzulu kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo jana jumapili.

Ozil alitoa maelezo hayo katika ukurasa wake wa mtandao Twitter jana jumapili.

“Kupiga picha ya Rais Erdogan halikua jambo la kisisasa, ilikua hatua kubwa kwangu kutokana kiongozi kuliongoza taifa la Uturuki ambapo ndipo asili ya wazazi wangu ilipo.”

Ozil amesema halikua jambo la busara kwa vyombo vya habari kutoa ushirikiano kwa wadau wa soka ambao walidhihirisha kuchukizwa na hatua ya kupiga picha na kiongozi huyo, bali ilitakia kuchukuliwa kama sehemu ya maisha ya kila siku.

Ozil alishambuliwa na kuingizwa katika tuhuma za kisiasa kufuatia mahusiano ya Ujerumani na Uturuki kuingia dosari July 2016, baada ya Rais Edogan kupinga baadhi ya mambo kutoka taifa hilo la Ulaya ya Magharibi.

Mapema mwezi huu meneja wa timu ya taifa ya Ujerumami Oliver Bierhoff, alikaririwa na vyombo vya habari akisema, walikua wanashinikizwa kumuacha Ozil katika kikosi kilichokwenda Urusi, kwa sababu za mchezaji huyo kupiga picha na kiongozi wa Uturuki, Lakini walitumia mamlaka yao kumjumuisha kiungo huyo.

Kwa upande wa Gundogan ambaye alishiriki katika picha ya pamoja na Rais wa Uturuki, amesema ni upuuzi na ujinga kwa baadhi ya mashabiki kuchanganya mambo ya soka na siasa, kwa kutumia kigezo cha picha.

TFF yazikumbusha klabu kufanya usajili
LIVE: Rais Magufuli akipokea Magawio kutoka Makampuni, Taasisi za Umma

Comments

comments