Mesut Ozil amesisitiza kwamba sasa ataipata jezi namba 10 baada ya Jack Wilshere ambaye ndiye alikuwa akiivaa kujiunga na Bournemouth kwa mkopo wa msimu mzima.
Kiungo mshambuliaji huyo raia wa Ujerumani, amekuwa akivaa namba 11 tangu alipowasili klabuni hapo akitokea Real Madrid mwaka 2013 kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi klabuni hapo.
Wilishere alipewa jezi namba 10 baada ya kuondoka kwa Robin van Persie ambaye ndiye alikuwa akivaa kuhamia klabu ya Manchester United.
Hivi karibuni Ozil pia ameichukua jezi namba 10 kwenye Timu ya Taifa ya Ujerumani baada ya Lucas Podolski kustaafu kuchezea taifa hilo.
“Kwangu mimi, jezi namba 10 ina maana kubwa sana,” Ozil alisema wakati akihojiwa juu ya jezi namba 10 ya Ujerumani. “Ni namba ninayoipenda kuliko zote. Manguli wa soka kama Zinedine Zidane, Diego Maradona na Pele wamewahi kuvaa jezi zenye namba 10. Nina furaha sana juu ya jezi hiyo.
“Nilitaka kuipata jezi hii miaka michache iliyopita, lakini alikuwa akivaa Lukas Podolski na alikuwa amecheza mechi nyingi zaidi yangu. Lakini sasa nimeipata rasmi.
Alipoulizwa kama anataka kufanya hivyo na Arsenal pia kuichukua jezi hiyo iliyoachwa na Wilshere, Ozil alijibu: “Ndio, kwasababu haina mtu, basi naihitaji sana

– See more at: http://www.barakampenja.com/2016/09/ozil-anaitaka-jezi-ya-wilshere.html#more

Manchester United Wazidi Kuchachawa Baada Ya Mchezaji Wao Luke Shaw Kuenguliwa Timu Ya Taifa Ya England,Kuelekea Derby Na Watani Wao Man City
Chadema: Hatuhamii Dodoma