Kiungo kutoka nchini Ujerumani, Mesut Ozil huenda akawa kwenye mtihani mgumu wa kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal, chini ya utawala wa meneja mpya Unai Emery.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa hii leo na gezeti la The Mirror la nchini England zinaeleza kuwa, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, ameshindwa kumshawishi meneja huyo kutoka nchini Hispania, katika kipindi cha mazoezi ya timu, hali ambayo imemsababishia kukosa mchezo dhidi ya Bournemouth mwishoni mwa juma lililopita.

Imethibitika Emery hakupendezwa na uchezaji wa kiungo huyo, wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Crystal Palace uliomalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili mwishoni mwa mwezi uliopita, hivyo alilazimika kumtengea Ozil mazoezi maalum ambayo ameshindwa kufikia kiwango anachokihitaji.

Katika mchezo uliofuata dhidi ya Wolves, Ozil alishindwa kuamliza dakika 90 baada ya kutolewa kipindi cha pili, huku akionyesha hasira dhidi ya maamuzi hayo.

Emery anatajwa kuwa meneja mwenye tamaduni za kipekee katika ufundishaji wa soka, na mara kadhaa amekua haangalii jina wala ustaa wa mchezaji, zaidi ya kushupalia kwenye mazoezi ya timu, ili kujihakikishia kikosi ambacho kitacheza mchezo unaofuata.

BREAKING NEWS: Rais Magufuli akihutubia katika uzinduzi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Baba amuua kijana aliyemkuta na binti yake aliyepotea