Hatua ya mlinda mlango wa Young Africans Metacha Mnata kuandika ujumbe wa kuwatakia kila la kheir wachezaji na uongozi wa klabu hiyo, kupitia ukurasa wake wa mtandao ya kijamii ‘Instagram’,  imepokelewa tofauti na wadau wa soka nchini kote.

Metacha aliandika ujumbe huo, huku mambo yakiendelea kuwa mabaya ndani ya klabu ya Young Africans, ambayo usiku wa kuamki jana Jumatatu Kocha Cedrick Kaze na benchi lake la ufundi wakifutwa kazi.

Ujumbe huo umepokelewa kama hatua ya mlinda mlango huyo kuwaaga wachezaji wenzake na viongozi, huku ikidaiwa Metacha alifikia maamuzi hayo baada ya kupigiwa simu na Mwenyekiti wa klabu hiyo Dkt. Mshindo Msolla akimlaumu kwa kufungwa goli kizembe hali iliyopelekea kupata sare dhidi ya Polisi Tanzania.

Hata hivyo Metacha aliufuta ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, na haijafahamika kwa nini alifanya maamuzi ya kuuondoa.

Mpaka sasa Uongozi wa Young Africans haujasema lolote kuhusu ujumbe huo, na haijathibitishwa kama kweli Metacha ataachana na Young Africans katika kipindi hiki, ambacho wanaendelea kupigania ubingwa wa Tanzania Bara pamoja na Kombe la Shirikisho (ASFC).

'Jembe Ulaya' awashauri viongozi Young Africans
Rage: Simba SC wana haki ya kupewa alama tatu, magoli mawili