Mlinda mlango wa Young Africans Metacha Boniface Mnata ameseama atawachukulia hatua za kisheria waliozusha taarifa za yeye kusaini Simba SC.

Metacha ambaye kwa sasa yupo mjini Nairobi kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, amesema ameshutushwa na taarifa hizo za uzushi, ambazo zinaendelea kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, mlinda mlango huyo amesisitiza, kwa sasa ametingwa na majukumu ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’, lakini ameahidi atakapokua huru atamshitaki mmoja baada ya mwingine.

Ameandika yeye bado ni mchezaji halali wa Young Africans na ataheshimu na kufuata taratibu za klabu hiyo, hata kama itatokea anaondoka, lakini sio kwa kurupuka kwa namna inavyoelezwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kwa sasa niko bize na majukumu ya timu ya Taifa, lakini nitakapokamilisha basi nimekipanga kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote ambao wanaeneza taarifa za uongo kunihusu. Ila niweke wazi kuwa mimi bado ni kipa wa Yanga,”

Metacha amezushiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na Uongozi wa klabu ya Simba SC, hasa ikizingatiwa siku chache zilizopita aliingia kwenye matatizo na mmoja wa viongozi wa Young Africans, ambaye anadaiwa alimpigia simu na kumlaumu, kufuatia bao alilofungwa na Polisi Tanzania, katika mchezo wa Ligi Kuu mjini Arusha.

Katika mchezo huo Young Africans walilazimishwa sare ya bao moja kwa moja, hatua ambayo ilichochea kufukuzwa kwa Kocha Cedric Kaze na wasaidizi wake katika benchi la ufundi.

Samia: Umeme kukatika mwisho leo
Al Merrikh waomba CAF iingilie kati vipimo vya Corona