Serikali ya Mexico imeteketeza tani 50 za madawa ya kulevya ya methamphetamine katika eneo ambalo madawa hayo yanatengenezwa.

Jeshi la wanamaji la nchi hiyo limesema kuwa eneo hilo limegunduliwa na wanajeshi hao baada ya kufanya uchunguzi.

Ripoti za kijasusi zimeeleza kuwa tani za madawa ya kulevya yalikuwa yanatengenezwa katika mji wa Alcoyonqui katika maeneo ya milimani umbali wa kilomita 19 nje ya mji mkuu wa jimbo la Sinaloa.

Aidha, Jimbo hilo ndilo lililokuwa eneo la kufanyia kazi la Joaquin Guzman maarufu “El Chapo” ambaye aliongoza kundi la kihalifu lililokuwa na nguvu hadi kukamatwa kwake mwaka 2016.

Kesi yake itasikilizwa nchini Marekani baadae mwaka huu, ambapo tangu kukamatwa kwa “El Chapo” makundi mengine ya kutengeneza madawa ya kulevya jimboni Sinaloa na sehemu zingine za Mexico yameendeleza utengenezaji na uuzaji wa madawa hayo katika nchi za nje hasa Marekani.

Video: Makonda, Nape wavaana wapinzani kuhamia CCM
Video: Waacheni wasumbukao na mizigo waje kwangu- JPM