Watu wenye silaha wamevamia nyumbani kwa meya wa jiji la Tripoli nchini Libya, Abdelraouf Beitelmal na kumteka kiongozi huyo wa halmashauri ya jiji hilo.

Vyanzo vya karibu na familia hiyo vimeiambia BBC kuwa wavamizi walimpiga mtoto wa meya na kitako cha bunduki kabla ya kuondoka na baba yake.

Taarifa ya baraza la madiwani la halmashauri hiyo imeeleza kuwa wamesitisha kazi zote kwa lengo la kupinga hatua ya kutekwa kwa meya huyo. Ilieleza kuwa kitendo hicho ni sehemu vitisho dhidi ya viongozi na raia.

Hata hivyo, mkuu wa kitengo cha upelelezi katika ofisi ya mwendesha mashtaka wa Serikali, Sediq AlSour aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanamshikilia meya huyo kwenye selo za polisi kwa mahojiano.

Alsour hakueleza kwa undani sababu za kumshikilia huku akisisitiza kuwa hawahusiki na tukio la kumteka.

Hatua hiyo inaongeza mkakanyiko katika utawala na mgogoro wa Libya.

Video: Urusi yajaribu kombora linalofika kona zote za dunia
Wavamizi wasaka dhahabu kwenye shamba la mke wa Mugabe