Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ,amelishukuru Shirika la Maendeleo la Japani (JICA) kwa kukamilisha mradi wa Barabara na bustani moja iliyopo mtaa wa Samora jijini humo.
 
Mradi huo ambao ambao ulianza utekelezaji wake mwezi Desemba mwaka jana umekabidhiwa kwa halmashauri ya manispaa ya Ilala kwaajili ya kuendelea na shughuli mbalimbali za kijamii.
 
Aidha, baada ya kukabidhiwa mradi huo uliogharimu jumla ya shilingi milioni 840 amesema kuwa mradi huo utaondoa kero mbalimbali kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam pia kuliweka jiji katika muonekano maridhawa.
 
Ameongeza kuwa mradi huo umechukua nafasi kubwa ya maeneo ya maegesho ya magari, lakini umepelekea kuwa na muonekano mzuri kutokana na maboresho yaliyofanyika katika mtaa huo.
  • Makamanda Zimamoto wapanguliwa
  • Video: Usiyoyajua sakata la shamba la Sumaye, Uchunguzi ‘Makinikia’ almasi pasua kichwa
  • Wazee walalamikia malipo TASAF, wadai yasilipwe kwa mtandao
 
Hata hivyo, mwakilishi wa shirika la Maendeleo Nchini JICA Tanzania, Toshio Nagase amesema kuwa mradi huo utawezesha kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam

Serikali ya Zimbabwe yamkingia kifua mke wa Mugabe
Joh Makini aeleza kwanini video za hip hop ‘hazikiki sana’ YouTube